Jumatano , 15th Mar , 2023

KIUNGO wa Simba SC, Clatous Chama amechaguliwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF, kuwa mchezaji bora wa wiki wa Klabu Bingwa Afrika, baada ya kufanya vizuri katika mchezo wa nne wa makundi dhidi ya Vipers SC.

Chama amewashinda Ahmed Zizo wa Zamalek, Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns na Walid Sabbar wa Raja.