
Fainali ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA, inazidi kuwa tamu baada ya Alfajiri ya leo LeBron James kufunga pointi 32 na Kyrie Irving kuongezapoints nyingine 30 na kuipa Cleveland Cavaliers ushindi wa vikapu 120-90 Golden State Warriors katika mchezo wa tatu wa fainali hizo ambapo mshindi atapatikana kwa kushinda mechi nne.
Huo ni mchezo wa tatu na licha ya kichapo hicho, Golden State bado wanaongoza 2-1 ambapo mchezo wa nne katika fainali hizo utapigwa jumamosi huko Cleveland Ohio.
Mshindi wa fainali hiyo, anatakiwa kushinda mechi 4 kati ya saba maarufu kama best of seven na kama Golden State itaendelea kuruhusu Cavaliers kusawazisha, basi inaweza kujikuta ikiwa na kazi kubwa kutetea taji lake.