Jumamosi , 16th Jan , 2016

Muda mfupi baada ya kutangaza kustaafu kuichezea Taifa Stars, nahodha na beki wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ leo Jumamosi anatarajia kukabidhi barua rasmi ya uamuzi wake huo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Cannavaro amesema, amechoka kuichezea Stars kwani muda alioitumikia Stars unatosha hivyo ni wakati wa kuwaachia wengine waendelee kuichezea timu kwa mafanikio.

Cannavaro amesema, atakutana na washauri wake ili kuandika barua hiyo na baada ya hapo atafika ofisi za TFF kwa ajili ya kukabidhi barua kuwataarifu rasmi kwamba mimi amejitoa Stars ili atoe nafasi kwa wengine.

Cannavaro amesema, amepokea maoni mengi kutoka kwa wadau wa soka na wote wanataka abadili uamuzi ili niendelee kuichezea Stars lakini hilo halitawezekana.

Hiyo ni siku moja tangu atangaze kujiuzulu kuichezea timu hiyo baada ya Kocha Boniface Mkwasa kumpokonya unahodha na kumkabidhi Mbwana Samatta.

Samatta alitangazwa kuwa nahodha na Mkwasa mara baada ya kushinda uchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka Afrika.