Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi.
Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.
TFF pia inaamini ushirikiano wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano hayo na hii ni mara ya kwanza kihistoria Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za za Mataifa ya Afrika.