Jumamosi , 3rd Feb , 2018

Utabiri wa kocha wa Manchester City Pep Guardiola kuwa safari ya "Burnley ni ngumu" imeonekana kuwa sahihi baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa EPL uliomalizika jioni hii.

Guardiola alitoa kauli hiyo kwenye mahojiano kabla ya mchezo ambapo aliulizwa kuhusu mtazamo wake kwenye mchezo huo ambapo alijibu kuwa ni mchezo mgumu usiotabirika.

Katika mchezo wa leo Manchester City ambao ni vinara wa ligi walitangulia kwa bao la dakika ya 22 lililofungwa na Danilo Luiz da Silva kabla ya Berg Gudmundsson kusawazisha dakika ya 82.

Matokeo hayo sasa yanawafanya Man City kufikisha alama 69 kileleni huku wapinzani wao katika nafasi ya pili Manchester United wakiwa na alama 53 na wapo dimbani muda huu dhidi ya Huddersfield Town.

Endapo Manchester United watashinda mchezo wao watapunguza tofauti ya alama kutoka 16 hadi 13.