
Wachezaji wa timu tofauti tofauti za Bundesliga. Kwenye picha ndogo ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kansela Angela Merkel, ametoa ruhusa huku akivitaka vilabu vyote kuwaweka karantini wachezaji kwa siku 14 kabla ya kucheza mechi yoyote.
Bundesliga huenda ikawa ligi ya kwanza kati ya ligi tano kubwa barani Ulaya kurejea mapema baada ya kusimama tangu mwezi Machi kutokana na janga la Corona.
Awali ligi hiyo ilikuwa irejee Mei 15, lakini Jumatatu ya Mei 4, wakaweka wazi kuwa wamefanya vipimo kwa wachezaji na wafanyakazi 1,724 wa vilabu 36 vya Bundesliga na Bundesliga 2 na kukuta 10 kati yao wameambukizwa Corona.
Ikiwa tayari ligi kuu nchini Ufaransa imeshafutwa na PSG kupewa ubingwa, kwa upande wa England wao wanatarajiwa kuanza mazoezi Mei 18, wakati La Liga leo Mei 6, 2020 wachezaji wamerejea kwenye vilabu na kufanyiwa vipimo.
Kwenye Serie A pia nchini Italia, baadhi ya vilabu vimeshaanza mazoezi hivyo huenda ligi ikarejea hivi karibuni.