Amis Tambwe wa Simba akishangilia moja kati ya mabao yake 19 aliyoifungia timu yake nakuibuka mfungaji bora wa ligi kuu msimu wa 2013/2014
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Tanzania Silas Mwakibinga amesema kuwa ligi ya msimu huu uliomalizika April 19 mwaka huu ilikua bora kuliko ligi iliyopita
Mwakibinga amesema ubora wa ligi hiyo umetokana na ushindani uwanjani kwa timu kuonesha uwezo na pia uchache wa adhabu za kadi hivyo imedhihirisha kuongezeka kwa nidhamu
Aidha Mwakibinga ameongeza kuwa, ligi ya mwaka huu imekuwa na rekodi nyingi ambazo hazijawahi kutokea, kwa mfano:
Kawnza, bingwa wa mwaka huu ni Azam FC ambayo inachukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza.
Pili timu ngeni kabisa katika ligi hiyo Mbeya City imeleta changamoto katika ligi hiyo na kufanikiwa kumaliza ligi hiyo ikiwa nafasi ya tatu ikiziacha timu kongwe za Simba, Kagera sugar, Mtibwa na Coastal zikiambulia nafasi za chini
Mwakibinga amesema rekodi kubwa ni katika kufumania nyavu ambako msimu uliopita hakukua na mchezaji aliyeweza kufunga magoli matatu peke yake katika mchezo mmoja yaani Hat Trick lakini msimu huu zimefungwa Hat Nrick Nne ambapo mbili zimefungwa na Mrundi Amis Tambwe wa Simba na nyingine zikifungwa na Mrisho Ngasa wa Yanga pamoja na mshambuliaji hatari wa Mbeya city Mwagane Yeya ambaye aliifunga Azam FC katika mchezo ulioishia kwa matokeo ya mabao 3-3 hiyo ikiwa ni Hat Trick ya kwanza kufungwa kwa timu ya Azam FC ikiwa katika uwanja wake wa Azam Complex.