Jumatano , 10th Dec , 2014

Shirikisho la Ngumi nchini BFT limesema hivi sasa lina uwezo wa kuandaa mashindano makubwa nchini ili kuweza kukuza uwezo wa mabondia.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa BFT, Lukelo Wililo amesema chanzo cha michezo mbalimbali kufanya vizuri na kukua inatokana na miundombinu ya kimichezo hivyo kwa upande wao wanaamini kwa hatua waliyofikia baada ya kuwa na ulingo mpya itasaidia hata kwa mabondia hao kujiamini pale wanapo panda ulingoni kwa ajili ya kupambana.

Wililo amesema ulingo waliokuwa wakiutumia hapo awali ulikuwa unamfanya bondia kushindwa kujiamini pale anapokuwa jukwaani suala linalopelekea kufanya vibaya katika mashindano mbalimbali makubwa ya ndani na nje ya nchi.