Jumanne , 19th Apr , 2022

Bingwa wa michuano ya wazi ya Australian 2022 Ashleigh Barty ambaye alitangaza kuachana na mchezo wa tennis anatarajiwa kushiriki kwenye maonesho ya michuano ya golf mnamo mwezi july,2022

(Nyota wa zamani wa tennis Ashleigh Barty)

Barty mwenye umri wa miaka 25 atashiriki kwenye michuano hiyo sambamba na mwalimu wa Manchester City Joseph Pep Guardiola na bingwa wa kuogelea wa medali za dhahabu za Olimpiki mara 23, Mmarekani Michael Phelps.

"ni nafasi ya kipekee kushiriki na kujipima binafsi na kushinda, natumaini ushiriki wangu kwenye mashindano haya yataongeza hamasa na mwamko wa wanawake na wasichana wengi kuingia kushiriki kwenye mchezo wa golf duniani kote “amesema Barty

Barty, bingwa mara 3 Grand Slam alitangaza kustaafu kucheza tennis,tukio lililowastua wengi huku mwaka 2015 alipumzika kucheza tennis na kugeukia mchezo wa criketi ambapo aliichezea timu ya taifa ya Australia maarufu kama Southern Stars .