Ijumaa , 15th Apr , 2022

Baada ya klabu ya Burnley kutangaza kumfuta kazi kocha wao Sean Dyche baada ya kuhudumu katika viunga vya Turf Moor kwa takriban miaka 10, sasa rekodi ya kocha aliyedumu kwa muda mrefu katika klabu za ligi kuu ya England anayefundisha hadi sasa imebaki kwa Jurgen Klopp na Pep Guardiola.

(Aliyekua kocha wa Burnley Sean Dyche na kocha wa liverpool Jurgen Klopp)

Kocha wa liverpool Jurgen klopp sasa ndio kocha aliyedumu kwa muda mrefu katika klabu moja bila kuhama kwa makocha wanao endelea kufundisha katika ligi kuu ya engalnd hadi sasa akiwa amedumu kwa miaka sita hadi sasa tangu ajiunge na kalbu hiyo mwezi August mwaka 2015, huku pepe guardiola akiwa wapili baada ya kuhudumu katika klabu ya matajiri wa jiji la manchester manchester city kwa miaka 5 hadi sasa tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi July mwaka 2016.

Kocha Sean Dyche mwenye umri wa miaka 50 ndio alikua akishikilia rekodi ya kocha aliyekaa muda mrefu zaidi na timu moja bila kuhama katika Ligi ya Engalnd kabla ya mchezo wake wa mwisho wa wiki iliyopita akiambulia kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Norwich na mchezo ambao umefikisha tamati kibarua chake.

Dyche amekuwa kocha wa Burnley tangu Oktoba 2012 na baadaye kusaini kandarasi mpya iliyotarajiwa kumalizika mwezi september msimu wa mwaka 2025.