Jumatano , 20th Aug , 2014

Penati ya Shomary Kapombe iliota mbawa na ile ya Mhaiti Leonel Saint Preux iliokolewa na kipa wa El Merreikh.

Picha ya maktaba ya kikosi cha Azam FC kilichotwaa ubingwa msimu uliopita. Hii ilikuwa Jumapili ya Machi 30 mwaka huu dhidi ya Simba ambapo Azam walishinda 2-1

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Azam FC, jioni ya leo wameyaaga mashindano ya 40 ya Klab bingwa Afrika Mashariki na kati maarufu kama kombe la Kagame baada ya kufungwa na klabu ya El Merreikh ya Sudan kwa penati 4-3.

Katika mchezo huo wa Robo Fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali nchini Rwanda, si Azam wala El Merreikh aliyeweza kuona mlango wa mwenzake hivyo mchezo huo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati na beki Shomari kapombe na mshambuliaji raia wa Haiti Leonel Saint Preux kukosa penati zao.