Jumapili , 20th Apr , 2014

Timu ya Azam FC wamekabidhiwa kombe rasmi mara baada Kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 baada ya kutofungwa mchezo hata mmoja katika msimu huu wa ligi uliomalizika

Rais wa TFF,Jamal Malinzi akimkabidhi Kombe Nahodha wa Azam FC,John Bocco Adebayo

Timu ya Azam FC wamekabidhiwa kombe rasmi mara baada Kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 baada ya kutofungwa mchezo hata mmoja katika msimu huu wa ligi uliomalizika.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kuhitimisha ligi msimu huu dhidi ya JKT Ruvu na kuibuka washindi kwa goli
1-0,Kocha Msaidizi wa Azam FC,Kalimangonga Ongala amesema jitihada kubwa walizoziweka katika msimu huu ndio iliyopelekea kutwaa ubingwa msimu huu.

Mara baada ya kukabidhiwa kombe la ligi kuu ya Tanzania Bara Azam FC,Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF,Jamal Malinzi anasema ushindi huo kwa timu ya Azam ni ishara ya kukua kwa ushindani na anaamini watafanya vizuri katika michuiano ya kimataifa na TFF itaendelea kuwapa ushirikiano ili kufikia malengo