
Wachezaji wa KMC na Azam FC
Azam FC walilazimika kuwa na kazi ya kusawazisha mabao ya KMC ambapo John Sangija aliitanguliza KMC dakika ya 18 tu ya mchezo kabla ya Tafadzwa Kutinyu kusawazisha bao hilo dakika ya 45 na kufanya kipindi cha kwanza kimalizike kwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili KMC waliongeza bao la pili dakika ya 63 kutpitia kwa Rayman Mgungila. Donald Ngoma akaisawazishia Azam FC dakika ya 85 hivyo kufanya mchezo umalizike kwa sare ya 2-2.
Baada ya michezo 16, Azam FC sasa wamefikisha alama 40 wakiwa nyuma kwa alama 41 dhidi ya vinara Yanga wenye alama 41 katika mechi 15.