
Kwa upande wa Mwadui wanashuka dimbani kuwakaribisha wenyeji wa Mgambo Jkt mjini Shinyanga na wagonga nyundo Mbeya City wakiwa wenyeji wa African Sports Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika mechi za hapo jana Mabingwa wa ligi kuu ya soka tanzania bara yanga wameendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo kwa point 3 zaidi kufatia ushindi wa magoli 4 kwa 1 dhidi ya toto aficans ya jijini mwanza katika mechi iliyopigwa hapo jana katika uwanja wa taifa jijini Jijini Dar es Salaam.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Juma Abdul, Simon Msuva aliyefunga mawili na Amisi Tambwe huku Donald Ngoma akikosa Penati iliyookolewa na mlinda mlango wa toto africans.
Huko Sokoine Jijini Mbeya, Tanzania Prisons ikainyuka Simba Bao 1-0 lililofungwa dakika ya 60 na mohamed Mkopi na kuwaporomosha simba hadi Nafasi ya 4 huku wao wakipanda na kushika Nafasi ya 6.
Nako Kambarage,mjini Shinyanga, Stand United ikaichapa Majimaji FC Bao 3-0 kwa magoli mawili ya Elius Maguri huku Athanas akikamilisha bao la tatu na kuchupa hadi Nafasi ya 3 kwenye msimamo.
Mjini Tanga, Coastal Union, wameonja raha ya nadra ya ushindi baada ya Bao la Kipindi cha Kwanza la Yusuf Chuma kuwainua kidedea kwa kuichapa Kagera Sugar 1-0 na kupanda hadi Nafasi ya12.
Ligi hiyo inaendelea jioni ya leo ambapo ndanda wataikaribisha Azam fc katika uwanja wa Nangwanda sijaona mjini Mtwara, JKT Ruvu wataialika mtibwa sukari katika uwanja wa karume jijini Dar es salaam huku Mwadui wakishuka dimbani kuwakaribisha wenyeji wa Mgambo Jkt mjini Shinyanga na wagonga nyundo Mbeya City wakiwa wenyeji wa African Sports Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.