Akizungumzia kuelekea tukio hilo la kurudisha kwa Jamii,Afisa masoko wa Azam FC Tunga Ally amesema Azam FC inakuwa timu ya kwanza hapa nchini kufanya jambo hilo ambalo ni sehemu ya shukrani kwa mashabiki wote huku huduma hiyo itawahusu wananchi wote.
'' Kila tunataka kuanza msimu mpya wa Ligi kuu tumekuwa na kawaida ya kurudisha kwa jamii kwa kufanya shughuli za kutoa msaada kwa watu mbalimbali ambao wamekuwa na changamoto za kimaisha ama kifedha''amesema Tunga.
Kwa upande mwingine, katibu wa mashabiki wa Azam FC amesema kuwa hili ni jambo kubwa na kwa hapa Tanzania haijawahi kutokea hivyo mashabiki wa Simba na Yanga na kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata huduma huku wakijiandaa na msimu mpya wa mashindano wa 2024-25.
Tayari Azam FC wametangaza kuwa tamasha lao la AZAMKA 2024 litafanyika Jijini Kigali nchini Rwanda ambapo litaunganishwa na tamasha la klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda mnamo Jumamosi ya Agosti 03-2024