
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Baraka Kizuguto amesema, mchezo mwingine wa kiporo utamalizika siku ya Januari Mosi hapo mwakani ambapo Ndanda FC watawakaribisha Simba SC uwanja wa Nangwanda sijaona mjini Mtwara.
Mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuhitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Katika mechi hiyo, Azam FC inashuka dimbani ikiwa nafasi ya pili ikiwa na point 32 huku Mtibwa Sugar wao wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na point 27.