
Afisa habari wa Azam FC Jaffary Maganga amesema, hawawezi kucheza mechi nyingine tena maana michuano ya ligi kuu inaanza wiki ijayo hivyo kuwa na mechi wana uwezo wa kupata majeruhi suala ambalo litamchanganya kocha.
Maganga amesema, wataondoka na wachezaji wote walionao kambini ili kocha kuweza kuangalia viwango vya wachezaji vilipofikia tangu kuanza kwa mechi za maandalizi ya ligi hiyo.