Jumanne , 14th Jun , 2016

Klabu ya Azam FC imesema, katika zoezi la usajili watakuwa na utofauti kwani hawatasajili mchezaji yoyote wa ndani bali watawapandisha wachezaji wao walio ndani ya kikosi cha vijana chini ya miaka 20.

Afisa habari wa Azam FC Jaffery Iddy Maganga amesema, kuachwa au kubaki kwa mchezaji katika kikosi cha Azam FC wataanza Julai Mosi mwaka huu ikiwa ni pamoja na timu kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa an msimu ujao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Maganga amesema, Makocha pia wataungana na kikosi kwa ajili ya mazoezi Julai Mosi kwani wameshasaini mikataba na wamerejea nchini mwao Hispania kwa ajili ya kufanya maandalizi.