Sam Allardyce anauwezo wa kuwa Meneja mzuri wa timu ya taifa ya Uingereza, kwa mujibu wa bosi wake wa zamani katika klabu ya West Ham, David Gold.
Allardyce maarufu kama "Big Sam", ambaye kwa sasa ni meneja wa Sunderland, anaongoza orodha ya makocha, wanaowania kumrithi Roy Hodgson ambaye alijiuzulu, baada ya Uingereza kushindwa kufanya vizuri katika mashindano ya Euro2016 hivi karibuni.
Ripoti za wiki hii zilidai kwamba Allardyce atahojiwa kwa nafasi hiyo, lakini chama cha soka cha Uingereza hakijawasiliana naye mpaka sasa



