Jumatatu , 28th Sep , 2015

Kikosi cha wachezaji 24 cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kinatarajiwa kuingia kambini tarehe mosi Oktoba, kwa ajili ya mchezo wa kufuzu kombe la dunia dhidi ya Malawi Oktoba 9 mwaka huu.

Kikosi cha wachezaji 24 cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kinatarajiwa kuingia kambini tarehe mosi Oktoba, kwa ajili ya mchezo wa kufuzu kombe la dunia dhidi ya Malawi Oktoba 9 mwaka huu.

Kikosi hicho kina walinda mlango Ally Mustapha(Young Africans),Aishi Manula(Azam fc) na Saidi Mohammed (Mtibwa Sugar),wakati Walinzi ni Juma Abdul,Haji Mwinyi,Kelvin Yondan,Nadir Haroub (Yanga), Mohamed Husein Tshabalala,Hassan Isiaka(Simba) na Shamori Kapombe kutoka Azam FC.

Viungo ni Himid Mao, Mudathiri Yahaya, Frank Domayo, Farid Mussa(Azam fc), Salum Telela, Deus Kaseke, Simon Msuva(Yanga),na Said Ndemla(Simba) huku Washambuliaji ni John Boko(Azam fc), Rashidi Mandawa Mwadui fc, Ibrahim Hajibu (Simba), Mbwana Samatta,Thomas Ulimwengu(TP Mazembe) na Mrisho Ngasa (Free State Stars).

Akizungumzia kikosi hicho ambacho hakina mabadiliko na kile kikosi kilichocheza na Nigeria mapema mwezi huu kocha msaidizi wa Stars Hemedi Morocco amesema kikosi hicho bado ni kizuri na wasingeweza kubadilisha mchezaji labda viwango vyao vingeshuka au kuwa na majeruhi.