Jumatano , 31st Oct , 2018

Nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo amevunja ukimya na kuamua kusema ya moyoni kuwa yenye na nyota wa Barcelona Lionel Messi ndio wachezaji bora kwa zaidi ya miaka kumi na wanastahili heshima.

Cristiano Ronaldo

Akiongea na jarida la 'France Football' ambao ni waandaaji wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu Balon d’Or, Ronaldo amesema mara nyingi huulizwa swali juu ya nani bora kati yake na Lionel Messi lakini ukweli ni kuwa wao wawili ndio wachezaji bora katika miaka ya hivi karibuni.

Mbali na hilo Ronaldo aliongeza kuwa wapo wachezaji wengi wanatajwa kuwa bora lakini changanoto kuwa ni uwezo wa mchezaji husika kucheza katika kiwango cha juu kwa muda mrefu zaidi.

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi

''Wachezaji bora wapo wengi mfano Salah, Modric,  Griezmann, Varane na Mbappé lakini huwezi kuwa na uhakika sana juu ya kiwango chao maana ukiniuliza wachezaji wawili waliodumu katika kiwango bora kwa muda mrefu naweza kuwahesabu tu na ni mimi na Lionel Messi'', amesema.

Aidha Ronaldo amepingana na kauli za mashabiki na wachambuzi mbalimbali wanaosema zama zake zimekwisha kwa kusema yeye bado ni mchezaji bora na anaamini anastahili kushinda Balon d’Or ya mwaka huu.