Jumatatu , 2nd Aug , 2021

Mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya kikapu ya Marekani, Kevin Durrant ameendelea kuonesha bora kwenye michuano ya Olympic inayoendelea nchini Japan na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo kwenye michuano hiyo mikubwa duniani kwa kufikisha alama 354.

Nyota wa timu ya Marekani, Kevin Durrant.

Durrant amefikisha alama hizo wikiendi iliyopita wakati timu yake ilipoifunga timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech kwa alama 119 kwa 84 ambapo Durrant alifikisha alama 23 rebound 8 na assist 6 na kupelekea nyota huyo kufikisha alama 354 kwenye michezo 19 ya Olympic tokea 2012.

Alama hizo zimemfanya Durrant pia kumpiku nyota mwenzake wa timu ya taifa, Carmelo Anthony aliyekuwa amefunga alama nyingi kwenye timu hiyo, alama 336 ambapo alicheza kwenye awamu nne za michuano ya Olympic kuanzia 2008.

Durrant amefunga alama 156 kwenye Olympic 2012 na alama 155 kwenye Olympic ya mwaka 2016 na kumaliza michuano yote hiyo akiwa na alama 30 na kushinda medali ya dhahabu.

Licha ya kiwango kizuri alichoanza kukionesha, Durrant anasafari ndefu ya kuwafikia wafungaji bora wa muda wote kwenye Olympic, Mbrazil Oscar Schmidt mwenye alama 1,093 na Andrew Gaze wa Australia  mwenye alama 789 ambao walicheza Olympic kwa awamu tano.