
Tajiri mtata Dkt Louis Shika
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Oktoba 18, 2019, Dkt Shika, amekitaja kiasi anachokitarajia kukipata kwamba ni kiasi cha dola za Marekani bilioni 11.
''Ninashauri kwamba tufanye siku nyingine kwasababu sasa hivi ninapoongea hapa nipo Posta nashughulikia masuala hayo hayo na kiasi cha pesa ninachokitegemea ni Dolla za Kimarekani bilioni 11 na niko ofisi husika za malipo, nipo namsubiri mwenzangu afike'' amesema Dkt Shika.
Dkt Shika alijizolea umaarufu huo mwaka 2017, wakati wa zoezi la upigaji mnada wa nyumba za Lugumi, baada ya yeye kupanda dau hadi kufikia kiasi cha Shilingi milioni 900 na baadaye alipohojiwa yeye alidai kuwa hakusema milioni 900 bali alitamka 900 itapendeza zaidi.