
Picha ya mtu akipima macho
Katika maadhimisho hayo Mratibu Mwandamizi wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Leah Mbunda amesema bado kuna vitendo vingi vya kiunyanyasaji hususani kwa mtoto wa kike na mara nyingi kesi hizo zimekuwa zikitendwa hasa na watu wa karibu zaidi na watoto hawa pasipo kuzingatia athari za baadaye.
Kwa upande wao washiriki wamesema ili jamii izidi kuwaamini baadhi ya mabinti waliopata nafasi za uongozi kwenye serikali na taasisi mbalimbali hawana budi kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi, huku wengine wakishauri kuwepo kwa mafunzo endelevu kwa mtoto wa kike ili kumjengea uwezo pamoja wadau kuachilia fikra za mfumo dume ambao umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu.
Kauli mbiu ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ni "Tumwezeshe Mtoto wa Kike; Kujenga Taifa Lenye Usawa"