
Katika mwezi huu, tunahimizwa kufanya matendo ya wema, kusaidia wenye mahitaji, na kuwa na subira. Ramadhan ni fursa ya kujiimarisha kiroho na kimaadili, na kuonyesha upendo na mshikamano kwa familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Kila siku ya mfungo inatoa nafasi mpya ya kutenda mema, kuwa na shukrani kwa yale tuliyonayo, na kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa dhati.
EastAfricaTv na EastAfricaRadio, tunawatakia Waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.