Ijumaa , 3rd Jun , 2022

East Africa Television na East Africa Radio leo iliendelea na kampeni yake ya Namthamini kwa kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike, ambapo leo ilifika katika sekondari ya Twiga pamoja na Maendeleo katika kata ya Wazo, Tegeta.

Wanafunzi wa Sekondari ya Maendeleo.

Hadi kufikia leo kampeni hii imekwisha wafikia wanafunzi wa kike katika mikoa tofauti ipatayo 15 na shule 63, ikiwa ni juhudi za kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kike wanakuwa na mazingira mazuri shuleni.

Hedhi salama ni ajenda ambayo imekuwa ikiwagusa watu wote kwenye jamii hasa kwa watoto wa kike walioko shuleni. Kampeni ya Namthamini ya East Africa Television kwa kushirikiana na wadau wengine wameendelea na zoezi la kugawa taulo za kike kwa wasichana walioko shuleni.