Pele enzi za uhai wake akicheza soka.
Ndugu wawili Rudolf Dassler aliyekuwa mmiliki wa Puma na Adolf Dassler aliyekuwa mmiliki wa Adidas waliingia katika vita ya biashara na kutengana, baada ya Puma kufanikiwa kumpata Pele kwa ajili ya kutangaza viatu vyao.
Pele alipewa ofa ya $25,000 (Tsh milioni 58) kwa ajili ya kuvaa puma katika Kombe la Dunia kwa sharti moja tu, kabla ya mechi kuanza ainame kufunga kamba za viatu ambapo camera zote zitammulika na kupelekea viatu vya Puma kuonekana.
Baada ya Pele kufanya kitendo hicho mauzo ya viatu vya Puma yaliongezeka kwa 300% na kuweka rekodi ya mauzo kwa mwaka huo, na Pele akapewa ofa nyingine ya $100,000 (Tsh milioni 233) kuvaa Puma kwa misimu minne.