Jumatatu , 5th Aug , 2024

Mmiliki wa META Bilionea Mark Zuckerberg ameandika rekodi mpya ya kuwa mtu wa tatu kwa utajiri duniani, haya yanajiri baada ya thamani ya hisa kutoka kwenye kampuni yake kuongezeka kwa asilimia 6

Hisa moja kwenye kampuni ya META inatajwa kufika thamani Milioni moja na laki tatu (1.3 Milioni) kutokana na kupanda huko kumefanya Mark kufikia utajiri wa Trilioni 477

Mark anashikilia nafasi hiyo baada ya Elon Musk ambaye ni Bilionea namba moja Duniani akiwa na utajiri wa Trilioni 627, na wa pili ni Jeff Bezos akiwa na utajiri wa Trilioni 541

NB: Mchanganuo wote hapo juu ni kwa shilingi ya Tanzania kwa kuzingatia kiwango cha dola leo hii ambapo Dola moja ni sawa na 2680, (META) ni kampuni inayomiliki mitandao ya kijamii Kama vile Facebook, Instagram, Threads, WhatsApp na Messenger