Makka ilivyombadilisha Ommy Dimpoz

Ijumaa , 21st Mei , 2021

Safari ya mjini Makka nchini Saudia Arabia ya siku kadhaa alizozitumia msanii Ommy Dimpoz kwa ajili ya ibada inawezekana kuwa imebadilisha kwa kiasi kikubwa mtindo wa maisha kwa msanii huyo.

Msanii Ommy Dimpoz

Dimpoz tangu amerejea nchini ameonekana kuwa tofauti kuanzia muonekano wake wa mavazi na jumbe ambazo amekuwa aki-share kwenye mitandao yake ya kijamii ukilinganisha na hapo awali kabla hajaenda kuungana na waumini mbalimbali wakiislamu duniani kote kufanya ibada ya Umrah mwezi Mei 9.

Msanii Ommy Dimpoz

Moja ya ujumbe wake unasema; ‘Tusichoke kumuomba na kumtegemea Mwenyezi Mungu kila kitu kinawezekana chini ya Jua’.