
Picha ya mtu akiwa amelala
Taaarifa hiyo kutoka kwenye tovuti yao inaeleza kuwa nia ya kutangaza kazi hiyo ni kujua faida na hasara ya kulala ili kutoa ufahamu kwa jamii kuhusu usingizi.
"Tulitaka kujaribu nadharia kadhaa juu ya faida na hasara za kulala ili kuipa jamii yetu ufahamu na umuhimu wa usingizi, tunajua kwamba usingizi mrefu una faida tofauti lakini tunataka kujaribu hii, na tunahitaji msaada wako"
"Pia kushiriki katika majaribio haya ya kupima nadharia hii kama vile muda mzuri wa kulala, kuburudika na athari za kulala kwenye viwango vya juu" taarifa hiyo imeeleza
Kwa sasa wataanza kuajiri kikosi cha watu watano wenye weledi wa kulala usingizi na mwisho wa kutuma maombi ya kazi hiyo ni Mei 31 na litadumu kwa muda wa siku 30.
Vigezo vyake ni kuanzia miaka 18 na zaidi, wawe wanalala peke yao wakati wa usingizi, pia lazima wawe na ustadi mkubwa wa uandishi wa Kiingereza.