Ijumaa , 9th Feb , 2024

Tukizihesabu siku 5 kuelekea siku ya wapenda nao, wacha tukufahamishe ya kwamba ni muhimu kwa maamuzi ndani ya mahusiano kutolewa kwa makubaliano ya wote wa wawili, lakini swali letu ni kwamba ni kitu gani huwezi kufanya bila mwenza wako?

 

Wakati unafikiria hilo, wacha tukufahamishe ya kuwa itakuwaje tukikupa uwezekano wa kufanya jambo la faragha kama vile upakuaji wa mizigo bandarini ukiwa na mwenza wako?

Basi fahamu kuwa kwenye maswala ya #UJENZI na mtaalamu wa hizi kazi @basilisa_john ambaye leo hii anashehereka miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake, anafanya juhudi kukuletea kipindi ambacho kitazungumza kuhusu choo kilichopo kwenye muundo mpya.

Si ulizoe kuona choo cha mtu mmoja pekee, basi fahamu choo hiki kinawawezesha wenza kuwa pamoja kwenye jambo la faragha linalohitaji utulivu mkubwa kuwa pamoja.