Jumatano , 8th Jun , 2022

Kijana anayetambulika kwa jina la Stephen Kamau kutokea Kaunti ya Nyandarua nchini Kenya, amesalimisha misokoto ya bangi yenye thamani ya Tsh milioni 20 kanisani na kuichoma moto.

Stephen Kamau akichoma bangi kanisani.

Kamau anasema ana furaha baada ya kubadilika na kuwa mtu bora kwenye jamii na wala hajatuii na kuhisi amepata hasara.

Kamau alipongezwa na waumini waliokuwa kanisani kwa kuacha biashara ya kuuza bangi na kumtaka ashawishi vijana wengine kuacha kufanya biashara haramu.