Alhamisi , 31st Mar , 2022

Ni headlines za msanii Malkia Karen ambaye ameiomba Serikali kumpeleka mbali hitmaker wa ngoma ya sukari Official Zuchu kwa sababu anafanya wasanii wengine kukosa usingizi na kutafakari.

Picha ya Malkia Karen kushoto, kulia ni Zuchu

Malkia Karen ameshea ujumbe huo kwa kuandika "Naiomba Serikali Official Zuchu apelekwe mbali anatufanya hatulali wasanii wengine hatutali hatutafakari".

Zuchu ni moja kati ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri hapa nchini kwa sasa licha ya kuwa na muda mfupi kwenye game.