Zari alitumia 'Insta Story' ya mtandao wa kijamii wa Instagram, kuandika yaliyomtokea kisha akaifuta post hiyo na kwenda kuandika tena kwenye mtandao wa Twitter.
“Niruhusuni niongee Leo , 'Perfume' zangu nne za gharama nilizopokea kama zawadi kutoka kwa marafiki zangu wa Dubai, zimeibiwa katika ndege ya Kenya Airways, Perfume haikuwa sehemu sahihi za kushikwa ndiyo maana sitaweza kukaa kimya juu ya hili, Suti zangu mpya nilizotakiwa kuzivaa kesho kwenye mkutano nazo hazionekani”, ameandika Zari The Bosslady.
“Mmeniangusha sana Kenya Airways, nimekuwa muaminifu lakini mmekuwa mkinikosea kila mara, muda mwingine huwa nadharau tu lakini sio kwa leo inatosha sasa na mmeshanipoteza kama mteja wenu” ameongeza.
Baada ya Zari The Bosslady kuandika hivyo kwenye mtandao wa Twitter,
Shirika la Ndege hiyo lilimjibu kuwa.
“Mpendwa wetu Zari tunatamani wateja wetu wote wawe na uzoefu chanya, tumekufikia baada ya kusikia taarifa zako za safari, sisi kama uongozi tunaratibu usafiri wa hapa uwanja wa ndege ili kuweza kujenga kilichotokea na kwa unyenyekevu zaidi” wameandika shirika la Kenya Airways.


