Jumatano , 18th Mar , 2015

‘In my world’ ndio jina la ngoma mpya ya Ysl Jacques aka DJ green amemshirkisha King V ambaye asili yake ni Burundi lakini kwa sasa wote wanaishi Marekani

King V jamaa amekulia Marekani ambako ndio makazi yake kwa sasa akiendelea na shughuli zake za muziki. Ysl Jacques aka DJ green huyu ni mtanzania ila kwa sasa naye makazi yake ni Marekani ambako anafanya kazi zake za muziki pia kuwa DJ

Unapozungumzia vipaji vizuri ambavyo vinachipukia na vikipewa sapoti vinaweza fanya vizuri zaidi huwezi kuacha kumzungumzia kuwazungumzia hawa jamaa King V na Ysl Jacques aka DJ green, hata unamposikiliza sauti zao wakiimba nyimbo zao lazima utaelewa vipaji walichobarikiwa.

Akipiga story na EATV Rapa King V amesema kuwa wimbo wao wa ‘In my world’ unazungumzia mambo mbalimbali yanayotokea katika dunia ya sasa.

“Tuliamua kuimba wimbo huu wa ‘In my world’ baada ya kukaa chini na kutafakari mambo mbalimbali yanayotokea sasa katika dunia hii na ndipo tukaona tufikishe ujumbe wetu kwa kufanya wimbo wenye ujumbe huu” amesema Rapa King V

King V amesema kuwa wimbo wa ‘In my world’ kwa sasa upo katika audio ila baada ya muda mfupi watatoa video yake na itasambaa kote hadi kwenye social media.

“ Ysl Jacques a.k.a Dj Green anatumia Kiswahili anapoimba ila mimi nachanganya Kiswahili na kingereza katika kuimba maana naona kuchanganya lugha ndio Watanzania na watu wengine watatuelewa vizuri” amefunguka Rapa King V

Mbali na kuimba na kuwa DJ pia Ysl Jacques a.k.a Dj Green ni producer wa muziki ingawa ana umri wa miaka 14 lakini ana uwezo wa kufanya mixing na beat mbalimbali.