Jumamosi , 21st Jun , 2014

Msanii mkali wa muziki kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika chati mbalimbali Afrika Mashariki kupitia ngoma yake ya Johnnie, ametua nchini Kenya akiwa katika ziara yenye lengo la kuimarisha soko la muziki wake.

Yemi Alade

Ujio wa msanii huyu ni kupitia ziara ambayo ameipatia jina 'Africa Media', ambayo ina lengo la kuwapatia mashabiki nafasi nzuri ya kumfahamu zaidi yeye na kazi zake kupitia mahojiano ambayo atakuwa akifanya na vituo mbalimbali.

Yemi Alade ameanza rasmi kujikita katika muziki mwaka 2005 akiwa anafanya kazi na kundi la Noty Spices, na sasa baada ya Johnnie kuikamata Afrika vizuri, anatumia nafasi hii pia kuitambulisha kazi yake inayokwenda kwa jina Tangerine.