Jumatano , 19th Feb , 2014

Msanii wa Kenya, Wyre The Love Child, pamoja na Chameleone wa Uganda ni miongoni mwa wasanii wakali Afrika, walioingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya msanii bora wa kiume katika tuzo za muziki za dunia.

Wasanii hawa katika kinyanganyiro hiki, wanashidana na wasanii wakubwa kabisa katika ngazi ya kimataifa kama vile Jay Z, Kendrick Lamar, Chris Brown, Trey Songs na wengineo.

Katika tuzo hizi, mshindi atategemea idadi ya mashabiki aliyonao kutoka kona zote za dunia ambao watashiriki kumpigia kura mara nyingi wawezavyo kwa njia ya mtandao ili kuwawezesha kushinda.