Whozu, Tunda wamkaribisha mtoto wao 

Jumapili , 20th Jun , 2021

Baada ya kukana kwa muda mrefu kuhusu taarifa za ujauzito Whozu ameamua kuweka wazi suala hilo baada ya kupost picha na mpenzi wake Tunda anayeonekana akiwa mjamzito huku akiweka 'caption' ya kumkaribisha mtoto wao huyo mtarajiwa.

Picha ya Whozu na mpenzi wake Tunda

Ujumbe huo ambao ameuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram unaeleza kuwa "Karibu duniani mwanangu huku mimi na mama yako tunakusubiri kwa hamu sana. leo ndio siku ya 'Baby Shower' yako, basi mwanangu mimi baba yako wala sina maneno mengi we chagua ufanane na mama yako au mimi utakavyopenda wala usijali

"Ila itapendeza sana mwanangu ukifanana na mama yako sababu 'She's So Beautiful' yaani ni pisi na nusu, eeh Mungu sisi sote tunajikabidhi mikononi mwako ikawe heri na faraja kwetu utulinde na wenye roho mbaya, roho za husda na wasiotupenda amen" ameongeza 

Aidha kwa upande wa Cappuccino Tunda ameandika "Siwezi kusubiri kuwa mama kwa kweli, mtoto yupo njiani".