Ijumaa , 27th Jun , 2014

Mwanamuziki wa pop wa Nigeria Adokiye ambaye pia ni balozi wa Umoja wa Mataifa ameibua mitazamo tofauti kwenye mitandao ya jamii baada ya kusema yupo tayari kujitoa yeye kwa Boko Haram ili waachiwe wanafunzi wasichana 276 iliyowateka.

Msanii wa muziki wa nchini Nigeria Adokiye

Adokiye ambaye ni msichana wa umri wa miaka 23, ametoa pendekezo hilo kwa jarida moja la Nigeria, ambapo kama hiyo haitoshi amesema yupo tayari kupoteza ubikira wake kama sharti la kuachiwa wanafunzi hao.

Mwanamuziki huyo ambaye pia ni muigizaji anayetokea jimbo la Imo, amesema amekuwa akiwawaza wasichana hao wadogo ambao wengine ni wenye umri wa kati ya miaka 11 na 12 na kushindwa kujua nini kinawatokea huko walipo.