Jumatano , 28th Oct , 2015

Onesho la kimataifa la msanii kutoka Nigeria, Wizkid Live In Dar litasindikizwa na wasanii, Diamond, Fid Q, pamoja na Christian Bella Jumamosi hii kwenye uwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa onyesho Solomon Nasuma akizungumza na waandishi wa habari

Akizungumza hii leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa onesho hilo Solomon Nasuma, amesema wamewachagua wasinii hao kutokana na kuwa na sifa ya kuweza kufanya show ya live, ambapo siku ya onesho hilo kutakuwa na Live Band kwa wasanii hao.

Katika kuonesha anajipanga vyema na show ya Live Band, msanii wa kimataifa wa Tanzania Nasib Abdul maarufu kama Diamond, alikuwa akijifua vyema kwa ajili ya mazoezi ya kufanya muziki wake Live na bendi.