Kilimanjaro Music Awards 2014
Tuzo hizi, kwa mwaka huu zimeweza kutoa nafasi kubwa kwa mashabiki kushiriki kikamilifu kabisa kuanzia hatua za awali kuchagua washiriki na baadaye kuwapigia kura kuamua ni nani ashinde na hivyo kuleta ladha zaidi kwa tuzo hizo mwaka huu.
Tukio hili kubwa litafanyika katika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, na habari nzuri kwako ni kwamba zitarushwa moja kwa moja kupitia Tinga nambari moja kwa Vinaja EATV kuanzia saa 3 kamili usiku.