Hayo yamesemwa na muongozaji wa video Khalfani, alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba wasanii wanafanya video na watayarishaji wa nje wakati hapa nyumbani wana uwezo.
"Hivi we unajua kwamba wasanii wa Tanzania ndio wanachangia asilimia nyingi tu kutushusha sisi, ila wakitaka kutupandisha tuwepo katika madirector wakubwa Afrika kama kina God Father inawezekana, kwa sababu sisi tuna uwezo wa kufanya vitu kama wanavyovifanya, ila tatizo linakuja kwenye bajeti", alisema Khalfani.
Khalfani aliendelea kusema kwamba tatizo jingine kubwa linalowafanya wasanii wasitumie waongozaji wa video wa hapa nyumbani, ni kutoamini uwezo wao na kwenda nje kutumia gharama kubwa.
"Unakuta hawatuamini kabisa, unakuta msanii anaenda kwa God father anaenda kumlipa milini 30 milioni 40 anaenda kufanya video, wakati hiyo video hata mi naweza kuifanya, alafu anakuja kwangu anakuja kulia bwana Halfani mimi sina hela, hizo video tunazozifanya zinatoka kali kwa uwezo wetu mkubwa tulionao wa kufikiria, vifaa sasa hivi vipo, kuna kila aina ya camera bongo sasa hivi", alisema muongozaji huyo wa video anayejulikana kwa jina Khalfani.