Ijumaa , 14th Aug , 2015

Katika kuelekea Uchaguzi mkuu mwezi Octoba mwaka huu zaidi ya wasanii 20 wanatarajia kuandaa wimbo mahususi kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

staa wa michano Profesa Jay

Staa wa michano Profesa Jay na wasanii wengineo wameiambia enewz kuwa lengo kubwa ni kuwahamasisha wanachi kutambua umuhimu wa kupiga kura kupitia tamasha lao la bure litakalofanyika jumapili hii kuanzia saa saba mchana likipambwa na mastaa Juma Nature, Ney wa Mitego, Kalajeremiah, Mh. Sugu, Flora Mbasha, Roma, na wengineo wengi.