Jumatatu , 24th Mar , 2014

Wasanii wa filamu hapa Bongo, mwishoni mwa wiki hii wanatarajia kufanya tukio kubwa Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuadhimisha miaka 3 tangu tasnia ya filamu Bongo ilipoanza kulikamata soko nchini, na kutoa heshima kwa wasanii waliokwishafariki.

Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere amesema kuwa,tukio hili ambalo litahudhuriwa na wasanii mbalimbali wakubwa na wadogo kutoka tasnia ya filamu, litapambwa pia na burudani ya muziki kutoka Bendi ya FM Academia, wasanii Linex, Shilole, Mr Nice na wengine.

Steve ameiambia eNewz kuwa, tukio hili litaenda sambamba pia na kutuza wasanii ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika tasnia hiyo, kujadili muelekeo wao katika sanaa na pia kufurahia wakati pamoja kama wanasanaa wenye mchango mkubw katika kuelimisha na kuburudisha jamii.

Tukio hili pia linatarajiwa kwa sehemu kubwa kufanya jazi ya kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya wasanii hawa wa filamu na pia kujenga ushirikiano utakaosaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo yao kwa ujumla.