Jumanne , 3rd Jun , 2014

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, ametangaza hatua za serikali kupambana na mmomonyoko wa maadili katika sanaa, kwa kufuta usajili kwa baadhi ya makundi ya burudani nchini.

Mh. Juma Mkamia

Naibu huyo ametoa onyo kwa baadhi ya wasanii ambao kazi na mionekano yao imeonekana kwenda kinyume na maadili.

Nkamia, ametolea mifano dhahiri ya baadhi ya waliochukuliwa hatua hii, likiwepo kundi la Kanga Moko pamoja na wasanii wa filamu na muziki, Ney wa Mitego, Wema Sepetu, Shilole pamoja na Aunt Ezekiel.