Jumamosi , 11th Jul , 2015

Rapa wa kike kutoka nchini Tanzania Chiku Keto amesema kuwa wanamuziki wa kike wanaofanya Hip Hop wanashindwa kutoboa kutokana na kubaniwa ngoma zao pamoja na wanawake wenyewe kuwa wepesi wa kukata tamaa.

Rapa wa Kike kutoka nchini Chiku Keto.

Chiku K amesema kuwa "madem" wanaofanya muziki wa Hip Hop kila wanapotoa ngoma hawapewi saporti ya kutosha hivyo kuwafanya krudi nyuma.

Pia Chiku K amesema kwa kuwa kwa sasa muziki wa kuimba ndiyo unaopewa sapoti ya kutosha sasa atakuja na style ya kuimba na kurap ili aweze kufanikiwa lakini endapo akishidikana basi ataaamua kuimba moja kwa moja.