Akiongea na 'EATV SAA MOJA' juu ya suala hilo, Naibu Wazir amesema Wema Sepetu tayari ameitwa na bodi ya filamu na kufanyiwa mahojiano kwa kusambaza picha zenye mahudhui ya kingono, na wasanii wengine ambao wamefanya makosa kama hayo pia watachukuliwa hatua.
Mhe. Shonza ameendelea kwa kusema kwamba mpaka sasa Baraza la Sanaa Tanzania, (BASATA) halimtambui mtu anayejiita 'Amber Ruti' kama ni msanii, kutokana na kutosajiliwa na baraza hilo.
Licha ya hayo Mh. Shonza amesema kwamba wasanii hao pia wataitwa na TCRA, huku akiwataka wasanii kutumia mitandao kuelimisha jamii badala ya kubomoa maadili na tamaduni za kitanzania