VIDE0 : Nitawashangaza wengi - Belle 9

Thursday , 18th May , 2017

Msanii wa muziki wa bongo fleva Belle 9 baada ya kumaliza matatizo ya msiba wa baba yake mzazi, amefunguka na kusema ujio wake sasa utawashangaza wengi kwani muda si mrefu anakuja na wimbo ambao utawashangaza wengi.

Msanii Belle 9.

Belle 9 amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha eNewz na kudai hiyo ngoma mpya inayokuja ni hatari sana kwani amefanya kitu cha tofauti sana.