Jumatano , 17th Apr , 2024

Mwana HipHop Roma Mkatoliki amewapiga dongo rappers wa sasa ambao hawawezi kuandika Verse 3 kwenye ngoma zao wakisingizia Radio hawataki nyimbo ndefu.

Picha ya Roma

“Nowdays Rappers wengi hawawezi kuandika verse 3. Excuse yao ni kuwa Radio hazitaki nyimbo ndefu but ukweli ni ngumu kwao kupata Lines (16x3) 48 Bars na kusimama kwenye Topic”.

“Zamani ma-brother walikuwa wanachora verse 3 na kila Verse wanapitiliza 16 Bars, unakuta verse moko linatoboa mpaka 32 huko”.

“Zali la Mentali Ya Prof verse ya kwanza ina kama 36 hivi au 40 na bado mtoto Viki ndo kwaanzaaa anaanza kumtongoza Ka’ Mkubwa”.