Jumatatu , 31st Mei , 2021

Baada ya kutikisa air waves na wimbo wake ‘Utawezana’ aliomshirikisha Mejja, Rapper Femi One kutokea nchini Kenya amefanikiwa kuachia album yake ya kwanza ‘Greatness’ yenye jumla ya nyimbo 14 na collabo kadhaa.

Msanii Femi One

Album hiyo imejumuisha nyimbo kama Adonai, Greatness, Mgongo, Duru, Wapewe na Jiongeleshe huku Mwamba wa Kaskazini Joh Makini, Bern Muziki, B2C, Zakah, Sanaipei Tande na Jay Rox wakiwa wameshirikishwa.

Mwaka 2019 Femi One aliachia Extended Play (EP) yake ya kwanza “XXV” ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa kwake kimuziki.